• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 3-March 9)

    (GMT+08:00) 2018-03-09 17:45:12

    Rais wa Zimbabwe aeleza wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya Mugabe na chama cha upinzani

    Chama kipya cha kisiasa kinachoaminika kuwa na uungaji mkono wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Bw Robert Mugabe kimeundwa ili kupambana na Rais wa nchi hiyo Emerson Mnangagwa kwenye uchaguzi utakaofanyika katikati ya mwaka huu.

    Taarifa iliyotolewa jana na chama cha New Patriotic Front imesema Bw Ambrose Mutinhiri amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama hicho na kuwa mgombea urais kwenye uchaguzi ujao. Bw Mutinhiri alikuwa ofisa mwandamizi wa jeshi na amejitoa kutoka chama cha ZANU-PF kupinga kuondolewa madaraka kwa Bw Robert Mugabe kwa njia isiyo ya kikatiba.

    Wakati hup huo Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema chama tawala cha ZANU-PF kina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti za vyombo vya habari zinazomhusisha rais wa zamani Bw. Robert Mugabe na chama kipya cha upinzani cha NPF.

    Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi hiyo vinaamini kuwa chama cha NPF kimeanzishwa na kikundi kinachoitwa G40 kinachoongozwa na mke wa rais wa zamani Bibi Grace Mugabe.

    Bw Mutinhiri amejitoa kutoka chama cha ZANU-PF na kujiuzulu ubunge ijumaa iliyopita, ili kupinga hatua alichoita kumwondoa madarakani rais wa zamani Robert Mugabe kwa isivyo halali. Halafu alikutana na Mugabe kwenye makazi yake huko Harare wikiendi iliyopita kumwarifu mpango wake mpya.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako