• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 3-March 9)

    (GMT+08:00) 2018-03-09 17:45:12

    Waziri mkuu wa Libya ataka jeshi liunganishwe kwa ajili ya usalama wa taifa

    Waziri Mkuu wa Libya anayeungwa mkono na umoja wa mataifa Bw. Fayez Serraj amesema kulinganishwa kwa jeshi la Libya ni muhimu kwa usalama wa nchi hiyo.

    Bw. Serraj amenukuliwa na vyombo vya habari vya Libya akiongea kwenye mdahalo wa kamati ya jeshi akisema, kuunganishwa kwa jeshi ni muhimu katika kulinda mipaka ya nchi na kukabiliana na changamoto ndani ya Libya.

    Kamati hiyo ilikuwa inamwarifu waziri mkuu kuhusu mazungumzo ya hivi karibuni ya Cairo, yenye lengo la kuleta umoja kwa majeshi ya Libya.

    Tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Rais wa Libya Muamar Gadaffi, Libya imekuwa na mgawanyiko kati ya eneo la magharibi na jeshi lake lililo chini ya Bw Serraj, na eneo la mashariki na jeshi lake lililo chini ya Kamanda Khalifa Haftar.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako