• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 3-March 9)

    (GMT+08:00) 2018-03-09 17:45:12
     

    Jeshi la Syria lapata maendeleo makubwa huko Ghouta Mashariki

    Serikali ya Syria imesema mapambano dhidi ya wapiganaji wa upinzani yanaendelea huko Ghouta Mashariki, pembezoni mwa mji wa Damascus, na jeshi la serikali limepata maendeleo makubwa kwa kudhibiti vijiji na mashamba kadhaa kwenye eneo hilo.

    Wakati huohuo, raia karibu 2,000 wameondoka katika eneo hilo.

    Serikali pia imesema wapiganaji wa upinzani walirusha makombora 300 dhidi ya maeneo karibu na Damasucs na kusabababisha vifo vya raia.

    Msafara wa magari ya kubeba misaada ya Umoja wa Mataifa umeingia kwenye sehemu zinazodhibitiwa na waasi, huko Ghouta Mashariki, pembezoni mwa Damascus, mji mkuu wa Syria.

    Malori 46 ya misaada yameingia wilayani Douma, ambayo ni ya kwanza kuingia eneo hilo tangu makubaliano ya kusimamisha vita kwa sababu za kibinadamu kutekelezwa siku 7 zilizopita.

    Kituo cha upatanishi cha Russia nchini Syria kimesema, waasi wa eneo hilo wameahidi kuwaruhusu raia kuondoka eneo hilo kwa sharti la kuingia kwa misaada hiyo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako