• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 7-Aprili 13)

  (GMT+08:00) 2018-04-13 15:40:28

  Rais wa Sudan aamuru kuachiwa huru kwa wapinzani wote wa kisiasa

  Rais Omar Al Bashir wa Sudan ametoa amri ya kuachiwa kwa wapinzani wote wa kisiasa wanaoshikiliwa nchini Sudan, kujibu mwito uliotolewa na vyama vya kisiasa.

  Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Sudan SUNA inasema uamuzi huo una lengo la kuhimiza moyo wa mshikamano wa kitaifa. Hatua hiyo pia imetajwa kuwa ni kufungua milango ya ushiriki wa kisiasa na majadiliano kuhusu mambo ya kitaifa na maandalizi ya kuandika katiba ya kudumu.

  Kuanzia mwezi Januari serikali ya Sudan imewaweka kizuizini wanasiasa wengi wa upinzani, kutokana na mwito waliokuwa wanatoa kwa wananchi kufanya mgomo kupinga ongezeko la bei kwa bidhaa za msingi, baada ya bajeti ya mwaka hii kupitishwa.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako