• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 7-Aprili 13)

  (GMT+08:00) 2018-04-13 15:40:28

  Watu 16 wafariki katika milipuko miwili mjini Mogadishu

  Watu 16 wakiwemo askari wawili wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika milipuko miwili tofauti iliyotokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

  Polisi na mashahidi wameeleza kuwa, mlipuko wa kwanza ulitokea katika kituo cha ukaguzi kando ya barabara karibu na uwanja wa ndege mjini humo baada ya gari iliyozuiwa na maafisa usalama wa kituo hicho. Askari watatu walijeruhiwa kwenye mlipuko huo huku mlipuaji wa bomu akifariki.

  Mlipuko wa pili ulitokea saa moja baadaye katika kituo kingine cha ukaguzi cha Sei Piano katika jimbo la Hodan magharibi mwa Mogadishu.

  Afisa wa polisi asiyetaka kutaja jina lake amesema askari wawili wameuawa baada ya vikosi vya usalama kuwaua wapiganaji watatu waliokuwa wakivuka katika kituo cha ukaguzi na gari iliyokuwa na vifaa vya mlipuko.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako