• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 21-Julai 27)

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:51:20

    Wapiganaji wa Al Shabab washambulia kambi ya jeshi kusini mwa Somalia

    Wapiganaji wa Al Shabab waliokua wamejihami kwa silaha za kivita wameendesha shambulio dhidi ya kambi moja ya jeshi kusini mwa Somalia, na kuua watu kadhaa, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi na mashahidi.

    Kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi katika eneo hilo, shambulizi hilo lililenga kambi ya kijeshi ya Bar-sanguni, kilomita 40 kaskazini mwa mji mkuu wa eneo hilo Kismayo.

    Washambuliaji wa kujitoa muhanga walifaulu kuingiza gari lao lililokua limejaa vilipuzi kabla ya wapiganaji wa Al Shabab waliokua wamejihami kwa silaha za kivita kushambulia kambi ya kijeshi. Ufyatulianaji risasi ulidumu muda wa saa moja

    Lakini wakati huohuo Jeshi la taifa la Somalia (SNA) na vikosi vya washirika jana vilifanya operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi la Al-Shabaab kwenye sehemu ya kusini nchini humo wiki hii, na kutwaa maeneo matatu karibu na mji wa bandari wa Kismayu.

    Kamanda wa jeshi la SNA kwenye eneo hilo Bw. Mukhtar Abdi Mohamed amesema, wapiganaji wawili wa Al-Shabaab waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa kwenye operesheni hiyo.

    Ameongeza kuwa lengo la operesheni hiyo ni kukomboa maeneo muhimu mengi zaidi yanayodhibitiwa na kundi la Al-Shabaab, vilevile amesema operesheni hiyo itaendelea hadi jeshi la SNA na vikosi vya Jubaland vitakapokomboa kanda hiyo nzima.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako