• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Julai 21-Julai 27)

    (GMT+08:00) 2018-07-27 18:51:20

    Mkutano wa 10 wa BRICS wakamilika Afrika Kusini

    Mkutano wa 10 wa nchi wanachama wa BRICS umekamilika wiki hii nchini Afrika Kusini.

    Akizungumza kwenye kongamano la biashara la kundi la BRICS linalojumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini lililofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China amesema mwongo ujao utakuwa muhimu sana ambapo waendeshaji wapya wa uchumi wa dunia watachukua nafasi ya wale wa zamani, mabadiliko ya kasi yatatokea kwenye mandhari ya kimataifa na muungano wa nguvu za kimataifa.

    Pia amesema dunia itashuhudia kujipanga upya kwa mfumo wa utawala wa dunia.

    Rais Xi amesema Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, pia ni sehemu yenye mustakabali mkubwa zaidi wa maendeleo duniani.

    Alisema China inapaswa kuimarisha ushirikiano na Afrika, kuunga mkono maendeleo ya bara hilo, ili kufanya juhudi za kujenga ushirikiano kati ya nchi za BRICS na bara la Afrika kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa ushirikiano kati ya kusini na kusini, na kufanya ushirikiano na nchi za Afrika katika kupunguza umaskini, usalama wa chakula, uvumbuzi, ujenzi wa miundo mbinu na maendeleo ya viwanda, ili kuchangia katika utekelezaji wa Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika.

    Naye rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia mkutano huo pia anafuatilia sana changamoto kubwa zinazoukabili utaratibu wa biashara ya pande nyingi, akisisitiza kuwa nchi za BRICS zinapaswa kulinda kwa pamoja utaratibu huo

    Alisema nchi za BRICS zimetambua bayana kuwa, zinapaswa kuhimiza utaratibu wa pande nyingi wa biashara ulio wazi, shirikishi na wenye kuwajibika ili kutoa mchango muhimu kwenye utaratibu huo.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako