• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 18-Agosti 24)

  (GMT+08:00) 2018-08-24 19:18:10
  Rais Xi Jinping wa China akutana na waziri mkuu wa Malaysia

  Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Malaysia Bw Mahathir Mohamad mjini Beijing.

  Rais Xi amempongeza Bw. Mahathir kwa juhudi zake kwenye kutilia maanani kuendeleza uhusiano kati ya nchi mbili, kuunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kutoa mchango katika kuhimiza ushirikiano wa kikanda wa Asia.

  Rais Xi amesisitiza kuwa China itaendeleza uhusiano wa kirafiki na Malaysia hasa katika zama mpya. Ametoa wito kwa nchi mbili kuheshimiana na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo, na kunufaishana kupitia ushirikiano wa kirafiki.

  Wakati huo huo, waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang pia amekutana na mwenzake wa Malaysia Bw Mahathir Mohamad, akisema China inapenda kuhimiza ujirani mwema na Malaysia. Ameongeza kuwa China inapenda kuunganisha pendekezo la "ukanda Mmoja, Njia Moja" na mkakati wa maendeleo ya Malaysia, na kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili kwenye sekta za biashara, uwekezaji, kilimo, uvuvi, miundombinu ya uchukuzi na nyinginezo.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako