• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 18-Agosti 24)

    (GMT+08:00) 2018-08-24 19:18:10

    Vikosi vya Usalama nchini Afghanistan vyapigana na kikundi cha wapigananaji waliojificha mjini Kabul

    Kikundi cha kijeshi kimevamia na kushikilia jengo moja na kuanza kuyashambulia majeshi ya serikali mjini Kabul nchini Afghanistan, jambo lilisababisha mapigano ya risasi.

    Hata hivyo, vikosi vya usalama viliyatambua maficho ya vikundi hivyo na kuanza kujibu mashambulizi ili kuhakikisha vinalinda amani ya Kabul.

    Kutokana na mapigano hayo, moja ya washambuliaji ameuawa na watu wengine wanne wamejeruhiwa.

    Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la polisi mjini Kabul Hashmat Stanikzai amethibitisha kuwa makombora yaliyorushwa kuelekea vituo viwili vya polisi vya Kabul lakini hakuna kifo chochote kilichotokea.

    Mashambulizi hayo ya makombora mjini Kabul yamefanyika siku moja baada ya rais wa Afghanistan Mohammad Ashraf Ghani kutangaza amri ya kusimaimisha mapigano kwa muda wa miezi mitatu kuanzia siku ya jana jumatatu, ikiwa ni siku moja kabla ya Eid-ul-Adha ambayo ni sikukuu ya mwaka ya waumini wa dini ya kiislamu, na akiwataka Taliban pia kutii amri hiyo.

    Kwa mujibu wa raia wa Afghanistan, kikundi cha Taliban kimepinga tangazo hilo la serikali la kusimamisha mapigano kwa kurusha makombora kuelekea mjini Kabul. Na kwamba eneo ambalo linashikiliwa na Taliban ni karibu kabisa na majengo yakiwemo Wizara ya Ulinzi na Ikulu ya Rais.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako