• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Agosti 18-Agosti 24)

    (GMT+08:00) 2018-08-24 19:18:10

    Misri yawasamehe wafungwa 2,376 katika sikukuu ya Idd el Adha

    Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema serikali imewasamehe na kuwaachia huru wafungwa 2,376, ikiwa ni pamoja na wadaiwa 627, ikiwa ni sehemu ya sherehe za sikukuu ya Idd el Adha. Msamaha huo umetolewa kwa amri ya Rais Abdel Fattah al- Sisi, baada ya uchunguzi kufanywa na kamati maalum.

    Kuachiwa wafungwa ni desturi ya serikali ya Misri ambayo hufanya hivyo kwa kuwaachia huru au kwa masharti, wakati sikukuu za taifa au sikukuu za kidini. Mwezi juni wakati wa msimu wa Ramadhani, Misri pia iliwaachia huru wafungwa 3,477.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako