• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 13-Oktoba 19)

    (GMT+08:00) 2018-10-19 19:43:20

    Rwanda Paul Kagame amwachisha kazi waziri wa ulinzi

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri na kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za nje.

    Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame amepoteza wadhifa wake kama waziri wa ulinzi na badala yake akateuliwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama.  

    Katika mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8 kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara ya ulinzi ambayo sasa inaongozwa na Meja jenerali Albert Murasira aliyechukua nafasi ya Jenerali James Kabarebe.

    Jenerali Kabarebe ambaye amepewa nafasi ya kuwa mshauri maalumu wa rais wa maswala ya ulinzi na jeshi alikuwa mshirika wa karibu sana na Rais Paul Kagame tangu vita vilivyong'oa utawala wa rais Juvenali Habyarimana miaka ya 1990.

    Jenerali Kabarebe ndiye mtu aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi ya nchi mbili Rwanda na Congo wakati wa utawala wa hayati Laurent Desire Kabila; kabla ya kuwa waziri wa ulinzi wa Rwanda kuanzia mwaka 2010.

    Mwanajeshi huyo ni miongoni mwa maafisa saba wakuu wa Rais Kagame ambao walikuwa wamefunguliwa mashtaka na Ufaransa kuhusiana na kuuawa kwa aliyekuwa rais Juvenal Habyarimana, mauaji ambayo yanadaiwa kuanzisha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 waliuawa, wengi wao Watutsi walio wachache.

    Hakuna sababu iliyotolewa ya kuondolewa kwa Kabarebe kutoka kwenye wizara ya ulinzi lakini, kuondoka kwake kunaonekana kama hatua kubwa katika kutaka kurejesha tena uhusiano mwema kati ya rwanda na Uganda.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako