• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 17-Novemba 23)

    (GMT+08:00) 2018-11-23 19:02:22

    Msuya ateuliwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa kuwa kaimu kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira, UNEP.

    Bi Msuya amekuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo ambalo lina makao makuu yake jijini Nairobi, Kenya.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amenukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa akisema Antonio Guterres amechukua hatua hiyo huku akiendelea kumtafuta mkuu wa kudumu wa UNEP.

    Wadhifa wa kiongozi wa UNEP ulikuwa umebaki wazi baada ya kujiuzulu kwa Erik Solheim ambaye amekumbwa na kashfa kuhusu gharama yake ya matumizi katika safari.

    Mswada wa ripoti ya ukaguzi wa, inaonyesha Solheim alitumia jumla ya $488,518 (£382,111) akisafiri siku 529 kati ya siku 668.

    Alikuwa hayupo afisini kwa takriban asilimia 80 ya muda wake kazini.

    Ripoti hiyo inasema gharama hiyo imetia doa sifa za UN kama shirika ambalo huangazia masuala ya uhifadhi wa mazingira na uendelevu.

    Solheim amesema anatumai hatua yake ya kujiuzulu italifaa shirika hilo, na Umoja wa Mataifa kwa jumla.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako