• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 17-Novemba 23)

  (GMT+08:00) 2018-11-23 19:02:22

  Bunge la Ethiopia lamteua kiongozi wa zamani wa upinzani kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi

  Baraza la makabwela la Bunge la Ethiopia limemteua kiongozi wa zamani wa upinzani Bibi Birtukan Mideksa kuwa mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo. Bibi Mideksa anachukua nafasi ya Samia Zekaria aliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo kwa mwaka mmoja uliopita.

  Uteuzi wa Bibi Mideksa unafuatia kurudi kwake nchini Ethiopia mwezi uliopita, baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Abiy Ahmed kutoa mwito wa kuleta mapatano kwa viongozi wa zamani wa upinzani, wakosoaji wa serikali na wanahabari waliokimbilia uhamishoni kutokana na tofauti kati yao na serikali ya Ethiopia.

  Vyama vya upinzani na watu wa kawaida wamekuwa wakitaka tume hiyo kutofanya upendeleo kwenye chaguzi, ambazo mara kwa mara zimekuwa ndio chanzo cha migongano kati ya waungaji mkono wa serikali na wapinzani.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako