• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 8-Desemba 14)

  (GMT+08:00) 2018-12-14 19:49:39

  Majengo ya tume ya uchaguzi yateketea DRC

  Majengo yanayotumiwa na tume ya taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yameshika moto na kuteketea mjini Kinsasa.

  Moto huo ulizuka mwendo wa saa nane usiku wa manane na kuzua taharuki ikizingatiwa kwamba ni siku chache tu zilizosalia kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.

  Moshi mweusi ulitanda angani na uliweza kuonekana kutoka mbali asubuhi kulipopambazuka.

  Moto huo unadaiwa kuathiri majengo ambayo yamekuwa yakitumiwa kuhifadhi vifaa vya uchaguzi.

  Chanzo cha moto huo bado hakijabainika.

  Waziri wa mambo ya ndani Henri Mova Sakanyi amesema uharibifu uliotokea ni mkubwa mno.

  Duru zinasema kulikuwa na mashine takriban 7,000 za kupitia kura ziliharibiwa.

  Uchaguzi nchini DR Congo utafanyika 23 Desemba.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako