• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 8-Desemba 14)

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:49:39

    Ali Bongo Ondimba aruhusiwa kuondoka hospitali

    Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameruhusiwa kuondoka hospitali ya kijeshi ya Rabat nchini Morocco ambako aliwasili mwishoni mwa mwezi Novemba.

    Kwa sasa Ali Bongo Ondimba ataendelea kupatiwa matibabu akiwa katika makazi binafsi katika mji mkuu wa Morocco.

    Kuondoka kwake ni uamuzi uliochukuliwa baada ya idhini ya timu ya matibabu, kulingana na vyanzo hivyo.

    Siku ya Jumatatu Ali Bongo alionekana hadharani kwa mara ya kwanza, akiwa na Mfalme wa nchi hiyo Mohammed VI aliyeenda kumtembelea.

    Siku ya Jumatatu jioni viongozi wakuu nchini Gabon, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu na Makamu wa rais walifanya safari kwenda kumjulia hali rais wa nchi hiyo Ali Bongo Ondimba anaendelea kupatiwa matibabu katika mji mkuu wa Morocco, Rabat.

    Makamu wa rais wa Gabon Pierre Claver Maganga, amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa, rais Ali Bongo anaendelea vema na hivyo hakuna ya kuwa na wasiwasi.

    Ugonjwa unaosumbua, haujawekwa wazi lakini, inaaminika kuwa alipata kiharusi mwishoni mwa mwezi Oktoba, wakati alipokuwa amekwenda nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kimataifa.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako