• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 8-Desemba 14)

  (GMT+08:00) 2018-12-14 19:49:39

  Waziri mkuu wa Ethiopia aeleza dhamira ya kuwafikisha mbele ya sheria wanaokiuka haki za binadamu

  Waziri mkuu wa Ethopia Bw Abiy Ahmed ameeleza dhamira ya kuwafikisha mbele ya sheria watu wanaokiuka haki za binadamu, ikiwa ni sehemu ya vita dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu.

  Bw Ahmed ametoa taarifa akisisitiza mageuzi yanayofanyika hivi sasa nchini Ethiopia ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kuwafikisha wahalifu mbele ya sheria.

  Amesema mageuzi makubwa yatafanyika serikalini, na wafungwa na raia watalindwa. Amesema vitendo vya zamani vya kukiuka ubinadamu havitatokea tena katika utawala wa sasa.

  Kabla ya hapo, maofisa wawili wa ngazi ya juu kutoka Shirika la ujasusi na usalama la Ethiopia NISS walikamatwa, kutokana na tuhuma za kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu katika miaka kadhaa iliyopita.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako