• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 22-Desemba 29)

  (GMT+08:00) 2018-12-28 20:00:53

  Zaidi ya watu 400 wauawa na tsunami nchini Indonesia

  Zaidi ya watu 400 wameuawa wiki hii na wengine 745 kujeruhiwa baada ya tsunami kukumba miji ya pwani nchini Indonesia kwa mujibu wa serikali.

  Msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa nchini Indonesia Supoto Purwo Nugroho amesema kuwa, maafa ya tsunami yamesababisha watu 21,921 wanaoishi kando ya maeneo ya pwani kuziacha nyumba zao, ikilinganishwa na jumla ya watu 16,082 siku ya jumanne.

  Timu za uokoaji nchini Indonesia zinafanya juhudi kufikia vijiji sita huko Sumur, huku helkopta zikitumika kwenye uokoaji, kutafuta na kuokoa waathirika wa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na tsunami nchini humo.

  Mawimbi ya tsusami yaliwasili usiku bila onyo lolote, na kuharibu mamia ya nyumba.

  Maafisa wanasema tsunami hiyo huenda ilisababishwa na maporomoko ya ardhi chini ya bahari baada ya kulipuka kwa volkano ya Anak Krakatau.

  Eneo la Sunda Strait kati ya visiwa vya Java na Sumtara huunganisha bahari ya Java na bahari ya Hindi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako