• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 22-Desemba 29)

  (GMT+08:00) 2018-12-28 20:00:53

  Al-Shabab yawaachia Wakenya wawili baada ya kuwashikilia kwa siku 5

  Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab la nchini Somalia limewaachia raia wawili wa Kenya baada ya kuwashikilia kwa siku tano tangu wiki iliyopita kutoka katika kijiji kaunti ya Wajir kanda ya kaskazini mashariki.

  Mkuu wa kanda ya kaskazini mashariki bw. Mohamed Birik amethibitisha kuachiliwa kwa raia hao bila ya mifugo yao baada ya kufanikiwa kwa makubaliano kati ya koo mbili za Somalia.

  Barik ameeleza kuwa, Serikali imeimarisha ulinzi na usalama katika miji ya mipakani kuzuia mashambulizi ya wanajeshi wa Al-Shabab.

  Birik amewataka wananchi kuwa makini na kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kusaidia kutokomeza makundi ya kigaidi yanayoongozwa na Al-Qaeda.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako