• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 2-February 8)

  (GMT+08:00) 2019-02-08 16:30:59

  Watu watano wafariki kutokana na shambuzi la kigaidi mjini Mogadishu

  Watu watano wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mlipuko wa gari uliotokea katika moja ya maduka makubwa katika mtaa wa Hamarwayne kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

  Afisa wa polisi Mohamed Abdulle amesema, bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari lililipuka katika mlango mkuu wa kuingia katika duka hilo karibu na makao makuu ya ofisi ya utawala Banadir na kuharibu majengo kadhaa.

  Kundi la Al-Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo.

  Agosti 2011 Jeshi la Somalia likisaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika waliwaondoa kundi la Al-Shabab kutoka kwenye mji wa Mogadishu, lakini kundi hilo bado lina udhibiti wa baadhi ya maeneo ya kati na kusini mwa Somalia na kuweza kufanya mashambulizi.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako