• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 2-February 8)

  (GMT+08:00) 2019-02-08 16:30:59

  Watu 26 wafungwa kwa hatia ya kuhamasisha vyombo vya habari vinavyoipinga serikali ya Misri

  Shirika la habari la Misri MENA limeripoti kuwa mahakama ya nchi hiyo imewahukumu watuhumiwa 26 wakiwemo 19 wanaokimbia, kifungo cha miaka 5 hadi 15 kwa hatia ya kuhamasisha na kufanya kazi kwenye vyombo vya habari vilivyo nje ya nchi, vinavyoliunga mkono Chama cha Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku.

  Mahakama ya makosa ya jinai ya Giza imewahukumu washitakiwa watano kifungo cha miaka 15, na wengine 21 kifungo cha miaka mitano, na kutangaza wawili kati ya watuhumiwa wengine 28 wanaohusika na kesi ya "vyombo vya habari vya Brotherhood" kuwa hawana hatia.

  Wengi wa watuhumiwa hao wanazihudumia stesheni za televisheni zinazoliunga mkono kundi la Muslim Brotherhood kutoka Qatar na Uturuki, ikiwa ni pamoja na Al Jazeera, Al Sharq na Mekameleen, ambao wanashtakiwa kujiunga na "baraza la mabadiliko ya Misri" kwa lengo la kuzuia na kudhuru taasisi za serikali ya Misri.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako