• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 2-February 8)

  (GMT+08:00) 2019-02-08 16:30:59

  Ufaransa yamwita nyumbani balozi wake wa nchini Italia kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara

  Ufaransa imemwita nyumbani balozi wake wa nchini Italia kwa mashauriano zaidi kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara yasiyo na msingi kutoka kwa maofisa wa Italia, na kuitaka nchi hiyo kurejesha uhusiano wao wa kirafiki na wa kuheshiminiana.

  Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetoa taarifa kuwa katika miezi kadhaa iliyopita Ufaransa imekuwa ikilengwa kwa mashambulizi hayo pamoja na kutoa taarifa za kukasirisha.

  Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Naibu waziri mkuu wa Italia Luigi Di Maio alikutana na wawakilishi wa harakati ya "Fulana za Njano" tarehe 5 huko Paris. Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa imesema kuwa kitendo hicho cha uchochezi hakikubaliwi na Umoja wa Ulaya na nchi jirani zake.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako