• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February23-March 1)

  (GMT+08:00) 2019-03-01 16:23:01
  Moto wauwa 20 katika kituo cha treni Cairo

  Watu ishirini wamefariki dunia na wengine 40 wamejeruhiwa katika kisa cha moto kilichotokea Jumatano (Februari 27) katika kituo cha kati cjijini Cairo, nchini Misri, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Misri.

  Tukio hilo limetokea kabla ya saa nne saa za Misri wakati treni ambayo haikuwa na mabehewa ilipokosea barabara yake na kuangukia kwenye jengo nambari sita la kituo cha Kati cha Cairo.

  Hali hiyo ilisababiosha kutokea kwa mlipuko wa pipa la treni hiyo linalohifadhi mafuta ya Diesel na kusababisha mgahawa uliokuwa karibu na eneo hilo kuteketea kwa moto.

  Hata hivy moto huo ulizimwa haraka. Watu waliofariki duni na majeruhi wamepelekwa katika hospitali jirani. Ajali zhuwa zikitokea mara kwa mara nchini Misri. ajali za treni na mikasa ya moto husababisha maafa mengi kila mwaka nchini Misri.

  Mnamo mwezi Februari 2002, zaidi ya watu 300 walifariki dunia baada ya treni waliokuemo kuteketea kwa moto.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako