• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February23-March 1)

  (GMT+08:00) 2019-03-01 16:23:01

  Umoja wa Mataifa wakataa miswada iliyotolewa na Marekani na Russia kuhusu suala la Venezuela

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kupitisha miswada miwili ya utatuzi wa suala la Venezuela iliyotolewa na Marekani na Russia.

  Mkutano uliofanyika ni wa tatu ulioitishwa na baraza hilo kuhusu suala la Venezuela ndani ya mwezi mmoja, kutokana na ongezeko la hali ya wasiwasi katika nchi hiyo ya Latin Amerika, tangu spika wa bunge Bw. Juan Guaido ajitangaze kuwa rais wa mpito tarehe 23 mwezi Januari na kutambuliwa na nchi kadhaa ikiwemo Marekani.

  Baada ya kura kuhusu miswada hiyo, naibu wa mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesisitiza kuwa, mambo ya Venezuela yanapaswa kuamuliwa na wananchi wake.

  Amesema China inafuatilia hali ya nchi hiyo, na kuunga mkono serikali yake kujitahidi kulinda mamlaka, uhuru na utulivu wa nchi hiyo.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako