• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February23-March 1)

  (GMT+08:00) 2019-03-01 16:23:01

  Waasi wa zamani wa M23 warejea DRC

  Serikali ya Uganda imeanza kuwarejesha nchini DRC wapiganaji wa zamani wa kundi la M23 pamoja na familia zao, ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya waasi hao wa zamani na Serikali ya Uganda na DRC kurejea nyumbani kwa hiari.

  Jumanne ya wiki hii Uganda iliwarejesha wapiganaji zaidi ya 70, utawala wa Kampala ukisema wengi wa wapiganaji hao wamekubali kwa hiari kurejea pamoja na familia zaidi.

  Wapiganaji hawa wanarejea nyumbani ikiwa ni miaka 5 tangu kundi hilo lishindwe vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

  Wapiganaji hao walioandamana na jamaa zao kumi wamesafirishwa kwa ndege ya Umoja Mataifa kutoka uwanja wa Entebbe Jumanne Februari 26 kuelekea nchi yao.

  Hatua ya kuwarejesha nyumbani imechukuliwa chini ya mpango wa utekelezaji wa makubaliano yaliofanyika mwaka 2013 ukiwa moja kati ya mikakati ya kutatua mzozo wa vita katika eneo la maziwa makuu.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako