• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 30-Aprili 5)

  (GMT+08:00) 2019-04-05 19:41:00

  Kikosi cha uokoaji cha China chamaliza kazi nchini Msumbiji

  Kikosi cha uokoaji cha China kimefunga safari ya kurudi nchini China baada ya kumaliza kazi ya uokoaji nchini Msumbuji kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Idai.

  Licha ya kazi ya uokoaji, kikosi hicho kilitoa huduma za matibabu na kuua wadudu na vijidudu pamoja na misaada ya dawa, chakula na maji safi ya kunywa kwa watu walioathiriwa na kimbunga Idai.

  Kabla ya kuondoka nchini Msumbuji, waokoaji wa China walitoa msaada wa vifaa vya matibabu na uokoaji kwa wizara ya afya ya Msumbiji, na idara husika za mji wa Beira.

  Ofisa mwandamizi wa kazi ya uokoaji mjini Beira Bw. Usscne Isse ameishukuru serikali ya China kwa kupeleka timu ya uokoaji nchini humo baada ya kutokea kwa maafa ya kimbunga Idai.

  Katika nchi jirani ya Zimbabwe ambayo pia iliathirika, Waziri wa huduma za habari, uenezi na raido Bibi Monica Mutsvangwa amesema hadi sasa watu 268 wamefariki na mamia ya wengine hawajulikani walipo kufuatia kimbunga Idai.

  Akizungumza na waandishi wa habari Bibi Mutsvangwa amesema kazi za uokoaji zinaendelea na inakadiriwa kuwa miili zaidi ya watu waliofariki itagunduliwa.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako