• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 6-Aprili 12)

  (GMT+08:00) 2019-04-12 19:08:22

  Chama kikuu cha upinzani chakiri kushindwa katika uchaguzi wa Israel

  Chama cha The Blue and White, ambacho ni mpinzani mkuu wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kimekiri kushindwa katika uchaguzi wa nchi hiyo, lakini kimeapa kuhudumia kama mpinzani mkali wa kiongozi huyo wa mrengo wa kulia.

  Viongozi wakuu wanne wa chama hicho cha mrengo wa kati, walitoa hotuba kwenye vituo vikuu vitatu vya televisheni nchini Israel.

  Kauli zao zilikuja baada ya asilimia 99 ya kura zilizohesabiwa kuonesha kuwa chama cha Likud na chama cha Blue and White kikipata viti 35 kila upande.

  Lakini chama hicho cha mrengo cha kulia kimepata kura nyingi za kutosha bungeni na kumruhusu Netanyahu kuunda serikali ijayo ya muungano.

  Awali Netanyahu alitoa ujumbe mzito kuhusu masuala ya usalama kabla ya kupiga kura, suala lililogeuka kuwa moja kati ya masuala muhimu katika uchaguzi huo.

  Alitoa tangazo muhimu katika siku za mwisho za kampeni, akieleza kuwa serikali mpya itaondoa makazi ya wayahudi kwenye ukingo wa magharibi

  Makazi hayo yanatajwa kuwepo kinyume cha sheria, chini ya sheria za kimataifa, ingawa Israel imekua ikipinga hilo.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako