• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 6-Aprili 12)

  (GMT+08:00) 2019-04-12 19:08:22

  Waziri wa usalama wa Marekani Kirstjen Nielsen ajiuzulu

  Waziri wa Usalama wa Marekani, Kirstjen Nielsen amejiuzulu, wakati wimbi la wahamiaji kwenye mpaka wa Mexico linaendelea kuongeza hasira ya Donald Trump.

  Afisa wa utawala wa Trump amesema rais ameomba waziri Nielsen ajiuzulu na waziri huyo hakusita kutekeleza ombi hilo.

  Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Donald Trump ameandika: "Waziri wa Usalama anatarajia kujiuzulu kwenye nafasi yake na ningependa kumshukuru kwa kile alichofanya."

  Katika ujumbe wake mwingine kwenye Twitter, rais wa Marekani ameongeza kuwa Kamishna wa sasa wa Forodha na Ulinzi wa mipaka ya Marekani, Kevin McAleenan, atakaimu nafasi ya waziri wa usalama.

  Awali kituo cha televiseni cha CBS kilizungumzia kuhusu kujiuzulu kwa waziri wa Usalama Nielsen.

  Kirstjen Nielsen, 46, amekuwa akishikilia nafasi hiyo ya Waziri wa Usalama tangu mwezi Desemba 2017. Wizara yake ina jukumu la kutekeleza sera yenye utata ya Trump, kama vile mpango wa kujenga ukuta kwenye mpaka na Mexico na kutenganisha watoto wa wahamiaji na familia zao.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako