• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 11-Mei 17)

  (GMT+08:00) 2019-05-17 19:35:33

  Genge la uhalifu wa mtandao duniani lavunjwa

  Genge la uhalifu wa kimataifa linalotumia mtandao kuibia watu katika nchi mbali mbali duniani limevunjwa . Genge hilo linadaiwa kuiba dola milioni 100 kutoka kwa watu zaidi ya 40,000.

  Hii imefuatia operesheni kali ya polisi iliyofanyika katika mataifa ya Marekani , Bulgaria, Ujerumani , Georgia, Moldova na Ukraine.

  Genge hilo liliweza kuiba kwa watumiaji wa kompyuta zenye programu ya software unaofahamika kama - GozNym malware- iliyotengenezwa kwa lengo la kuvuruga, kuharibu au kuweza kuingia kwenye mfumo wa kompyuta bila idhini ya mtumiaji ambao ulinasa taarifa za huduma za benki za mtandao na hivyo kuweza kuingia kwenye akaunti za benki. Genge hilo liliwajumuisha wahalifu ambao walitangaza ujuzi wao wa kuiba kupitia mitandao mbali mbali. Taarifa juu ya harakati za kuvunja mtanao wa genge hilo zimetolewa katika makao makuu ya polisi ya shirikisho la polisi la Muungano wa Ulaya mjini The Hague Uholanzi. Miongoni mwa waathiriwa wa wizi wa genge hilo ni wafanyabiashara wadogo, makampuni ya sheria, Ushirikiano wa kimataifa na mashirika mengine.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako