• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 11-Mei 17)

  (GMT+08:00) 2019-05-17 19:35:33

  Zaidi ya watalii 200 kutoka China wapiga jeki sekta ya utalii Tanzania

  Zaidi ya watalii 200 kati ya 336 kutoka nchini China wametembelea Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro na kufurahia wanyama mbalimbali waliowaona kwenye shimo kubwa lililopo hifadhi hiyo maarufu kwa jina la Kreta.

  Watalii hao waliwasili katika hifadhi hiyo wakitokea kwa magari maalumu ya kitalii na kupokelewa kwa ngoma za asili za kabila la Kimasai na Watatoga.

  Baada ya kuingia lango kuu la hifadhi walionekana wakiwa na furaha, huku baadhi yao wakionekana wakipiga picha msitu mnene waliouona na wanyama.

  Aidha, walilazimika kushuka baadhi ya maeneo na kupiga picha kwenye miti mikubwa na magogo ya miti iliyolala. Baadhi ya watalii hao walihudhuria kongamano la uwekezaji lililofanyika ukumbi wa kimataifa wa mikutano AICC uliopo Mjini Arusha, huku wenzao wakitangulia Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.

  Mwenyekiti wa Kampuni ya Touchroard International Holdings Groups ya China, He Lei Hiu, amesema wamefurahishwa na ukarimu wa Watanzania na mapokezi makubwa waliopatiwa.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako