• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 8-Juni 14)

  (GMT+08:00) 2019-06-14 19:52:18

  Mtu wa pili afariki kwa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda

  Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kuwa mtu wa pili amefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola baada ya jumanne kutangaza kuwa nchi hiyo imekumbwa na ugonjwa huo.

  Watu waliokufa wanatoka kwenye familia ya watu sita waliosafiri kwenda katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, walikokwenda kumwuguza ndugu yao ambaye baadaye alikufa kwa ugonjwa wa Ebola.

  Mvulana mwenye umri wa miaka mitano na bibi yake waligunduliwa kuambukizwa virusi vya Ebola baada ya kurudi Uganda kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

  Hii ni mara ya pili kwa Uganda kutangazwa kukumbwa na homa ya Ebola, mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012, ambapo watu 20 walifariki.

  Serikali ya Uganda imewahakikishia watalii kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kufuatia mlipuko wa homa ya Ebola kuripotiwa nchini humo.

  Waziri wa nchi anayeshughulikia utalii Bw. Godfrey Kiwanda, amesema maambukizi ya mtu mmoja katika wilaya ya Kasese ni tukio la mtu mmoja tu, kwa kuwa wanafamilia wote wa mtu aliyeambukizwa wamefuatiliwa.

  Shirika la afya Duniani WHO limesema hakuna haja ya kutoa tahadhari ya kusafiri kwenda Uganda baada ya nchi hiyo kukumbwa na maambukizi ya mtu mmoja. Shirika hilo limesema watu wanatakiwa kujilinda. Vikundi vya wataalamu wa afya tayari vimetumwa na mlipuko wa Kasese utadhibitiwa.

  Wakati huohuo, WHO imesema inapeleka dozi 3,500 za chanjo ya Ebola nchini Uganda baada ya mtu wa kwanza kufariki kwa ugonjwa huo nchini Uganda.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako