• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 8-Juni 14)

    (GMT+08:00) 2019-06-14 19:52:18

    DRC yaitaka Uganda kudhibiti safari za kuvuka mpaka wa nchi hizo kukabiliana na Ebola

    Wahudumu wa afya katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambalo limeathirika zaidi na mlipuko wa Ebola, wameitaka Uganda kudhibiti safari za kuvuka mpaka wa nchi hizo ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo.

    Wizara ya Afya ya Uganda ilitoa taarifa wiki hii ikisema, wafanyakazi hao wametaka suala la safari za mara kwa mara za kuvuka mpaka zinazofanywa na watu waliokutana na watu wenye maambukizi ya Ebola zidhibitiwe.

    Wakati huohuo, Kenya imetoa tahadhari ya kiafya kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda. Waziri wa Afya nchini humo Bi. Sicily Kariuki amesema, Kenya imewataka wahudumu wake wa afya kuwa katika hali ya tahadhari, tayari kukabiliana na mlipuko huo kama utatokea.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako