• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 8-Juni 14)

    (GMT+08:00) 2019-06-14 19:52:18

    Umoja wa Afrika kukabidhi kambi ya jeshi kwa majeshi ya Somalia

    Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imesema inawasiliana na serikali ya Somalia na wadau wengine kuhusu kuanza kazi ya kukabidhi kambi za jeshi kwa idara za usalama za huko, ikiwa ni sehemu ya mpango wa mpito.

    Mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Francisco Madeira amesema tume hiyo kwa sasa imefika katika wakati muhimu kwenye utekelezaji wa mpango wa mpito, wa kukabidhi polepole majukumu ya usalama kwa majeshi ya Somalia.

    Bw. Madeira amesema katika miezi inayokuja AMISOM kwa kushauriana na serikali ya Somalia na wadau wengine, itakabidhi kambi ya operesheni kwa vikosi vya usalama vya Somalia.

    Bw. Madeira amesema hayo kwenye hafla ya kukabidhi majokofu sita ya makontena kwa vikosi vya usalama vya Somalia ili kuimarisha uwezo wake wa kuikomboa nchi kutoka kwa wapiganaji.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako