• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 20-July 26)

    (GMT+08:00) 2019-07-26 19:44:19

    Hugo Santillan: Bondia wa Argentina afariki kufuatia majeraha aliyopata katika pigano

    Bondia wa Argentina Hugo Santillan amefariki kutokana na majeraha aliyopata katika pigano , siku chache baada ya kifo cha bondia wa Urusi Maxim Dadashev.

    Bondia huyo mwenye umri wa miaka 23 alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare.

    Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi wiki hii. Santillan ni bondia wa pili kufariki kutokana na majeraha aliyopata katika ulingo wa ndondi wiki hii baada ya kifo cha Dadashev kuthibitishwa siku ya Jumanne.

    Bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 alipelekwa hospitalini akitokwa na damu katika ubongo baada ya pigano lake la IBF ukanda wa Welterwieght dhidi ya Subriel Matias kusimamishwa mwisho wa raundi ya 11 Ijumaa iliopita.

    Alifanyiwa upasuaji wa dharura lakini ukafeli.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako