• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 27-August2)

  (GMT+08:00) 2019-08-02 19:11:56

  Hoteli ya DusitD2 yafunguliwa baada ya zaidi ya miezi sita

  Hoteli ya DusitD2 iliyoko Riverside Drive, Westlands na ambayo ilishambuliwa na magaidi na kusababisha vya zaidi ya watu 21 ilifunguliwa Jumatano wiki hii baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi sita tangu shambulizi hilo lifanyike Januari 15, 2019. Sherehe za ufunguzi zilishuhudia kupandishwa bendera tatu na mwanariadha nguli David Rudisha na mkuu wa hoteli hiyo yenye matawi mbalimbali.

  Hoteli hiyo ambayo inamilikiwa na raia wa Thailand ilisalia imefungwa tangu tukio la shambulizi la kigaidi ambalo kundi la al-Shabaab lilikiri kuhusika.

  Hoteli hiyo ambayo imekodisha asilimia kubwa ya vyumba vilivyoko 14 Riverside Complex ilisalia imefungwa licha ya afisi za biashara nyinginezo kufunguliwa. Watu walianza kupata huduma katika hoteli hiyo kuanzia siku ya Alhamisi.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako