• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 27-August2)

    (GMT+08:00) 2019-08-02 19:11:56

    Saudi Arabia yawaruhusu wanawake kusafiri bila uangalizi

    Wanawake nchini Saudi Arabia wameruhusiwa kusafiri nje ya nchi bila kuandamana na wanaume.

    Chini ya sheria mpya iliyotangazwa ijumaa wiki hii , mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 21 anaweza kutuma maombi ya paspoti bila idhini ya mlezi wa kiume.

    Watu wazima wote wanaweza sasa kuomba paspoti na kusafiri hatua inayowapatia haki sawa na wanaume.

    Agizo hilo la ufalme pia linawapa wanawake haki ya kuwasajili watoto wao wanapojifungua, kufunga ndoa au talaka. Pia sheria hiyo mpya inazungumzia sheria za ajira ambazo zinapanua fursa kwa wanawake.

    Kwa mujibu wa sheria hiyo, raia wote wana haki ya kufanya kazi bila kubaguliwa kwa misingi ya jinsia, ulemavu au umri. Sheria hiyo mpya inakuja wakati ambapo mashirika ya kimataifa mara kwa mara yamekuwa yakidai kwamba wanawake wanachukuliwa kama raia wa daraja la tatu nchini humo.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako