• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 27-August2)

    (GMT+08:00) 2019-08-02 19:11:56

    Serikali na upinzani wasaini makubaliano ya amani Msumbiji

    Serikali ya Msumbiji na upinzani Renamo hatimaye wamesaini makubaliana ya kumaliza uhasama ambao umedumu kwa miaka na mikaka. Baadhi ya wafuasi wa Renamo wanaosalimisha silaha watajumuishwa katika jeshi na polisi. Kiongozi wa Msumbiji Filipe Nyusi na wa upinzani Ossufo Momade walisaini makubaliano hayo wakiwa na lengo la kumaliza rasmi miaka mingi ya uhasama.

    Makubaliano hayo yamesainiwa katika mbuga ya kitaifa ya jimbo la kati nchini Msumbiji, takriban miaka 27 tangu mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya taifa hilo la kusini mwa Afrika. Makubaliano hayo yaliyosainiwa Alhamisi, yanakamilisha mazungumzo ya amani yaliyoanzishwa na kiongozi wa chama cha upinzani Renamo Afonso Dhlakama aliyefariki mwezi Mei mwaka uliopita, na pia unajiri miezi miwili tu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako