• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 24-August 30)

  (GMT+08:00) 2019-08-30 18:48:16

  Askari 25 wauawa katika shambulizi la kundi la Houthi kaskazini mwa Yemen

  Askari 25 wa jeshi la serikali ya Yemen wanaoungwa mkono na Saudia wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kundi la Houthi lililofanyika katika mkoa wa Saada, kaskazini mwa nchi hiyo.

  Afisa wa kijeshi amesema, kundi la Houthi limevamia vituo kadhaa vya kijeshi katika eneo la Kataf, mashariki mwa mkoa wa Saada na kuwakamata askari kadhaa.

  Gavana wa mkoa wa Saada Bw. Hadi Tarshan amethibitisha kwamba, mapambano yameendelea kwa siku tatu mfululizo katika eneo hilo. Amesema vikosi vya serikali vimepeleka askari zaidi ili kusaidia wanajeshi katika mapambano hayo.

  Wiki hii pia ndege za kivita za muungano wa jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia zimeshambulia mara kadhaa uwanja wa ndege wa mji wa Sanaa, Yemen, ambao unakaliwa na waasi wa Houthi, saa moja tu baada ya waasi hao kurusha kombora dhidi ya uwanja wa ndege wa Abha wa Saudi Arabia.

  Ripoti iliyotolewa na televisheni ya al-Masirah inayoendeshwa na waasi wa Houthi zinasema, kombora hilo limelenga kituo cha operesheni za kijeshi na mabanda ya ndege.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako