• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 24-August 30)

  (GMT+08:00) 2019-08-30 18:48:16

  China yaitaka Marekani kusimamisha hatua ya makosa ya kuongeza ushuru

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng hapa Beijing amesema, timu za uchumi na biashara za pande mbili za China na Marekani zinaendelea kuwasiliana, na kuongeza kuwa ingawa Marekani itaahirisha kuongeza ushuru kwa baadhi ya bidhaa za China zinazouzwa nchini Marekani, lakini ushuru wowote mpya utasababisha kupamba moto kwa mikwaruzano ya kibishara kwa upande mmoja na kukiuka vibaya makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili huko Osaka.

  Bw. Gao amesema, kama Marekani itaendelea kuongeza ushuru, itabidi China kuchukua hatua ya kulipiza kisasi. Ameitaka Marekani kuacha makosa ya kuongeza ushuru na kuwa kwenye mwelekeo mmoja na China, ili kutafuta utatuzi juu ya msingi wa usawa na kuheshimiana. Hali hiyo itazinufaisha pande zote mbili na dunia nzima.

  Habari zaidi zinasema Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetoa makala kwenye blog yake likisema kuongeza ushuru hakuwezi kusaidia kutatua suala la biashara isiyo na uwiano kwa ujumla, badala yake, kutadhoofisha imani na uwekezaji wa makampuni, kuvuruga mnyororo wa utoaji wa bidhaa duniani na kuongeza matumizi ya watengenezaji na wateja na mwishoni kuzuia maendeleo ya uchumi wa nchi yenyewe na wa dunia nzima.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako