• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 26-Novemba 1)

  (GMT+08:00) 2019-11-01 20:45:37
  Uganda kutuma kikosi zaidi Somalia

  Kiongozi mmoja wa ofisi ya polisi nchini Uganda wiki hii alinukuliwa akisema kuwa Uganda imepanga kutuma polisi wengi zaidi kujiunga na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM).

  Mkurugenzi wa operesheni za kusaidia amani katika kikosi cha polisi cha Uganda Bibi Grace Turyagumanawe amesema kuwa Uganda inafanya maandalizi ya kutuma polisi zaidi ili kuunga mkono usalama wa Somalia.

  Bi. Grace alisema hayo alipokutana na naibu mjumbe maalum wa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika anayeshughulikia suala la Somalia Bw. Simon Mulongo mjini Mogadishu, aliongeza kuwa maandalizi yanaendelea ili kuhakikisha kupelekwa kwa polisi wa kundi la pili hivi karibuni.

  Kutokana na Mpango wa Mpito wa Somalia, polisi wa AMISOM wanafanya kazi kuhakikisha Jeshi la Polisi la Somalia kuwa na vifaa vya kutosha, ili liweze kuchukua jukumu kamili la kutekeleza sheria na kulinda utulivu nchini Somalia baada ya ujumbe wa AMISOM kuondoka mwaka 2021.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako