• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 26-Novemba 1)

  (GMT+08:00) 2019-11-01 20:45:37

  IS yamteua kiongozi mpya baada ya Badhdadi kufariki

  Kundi la kigaidi la wapiganaji la Islamic state hatimaye limemtangaza kiongozi wao mpya baada ya kiongozi wa zamani wa kundi hilo Abu Bakr al-Baghdadi kuaga dunia. limethibitisha kifo cha kiongozi wake na kumtangaza mrithi wake.

  Kwenye ujumbe wake, kundi hilo la kijihad limemteua Abu Ibrahim al-Hashemi al-Qurayshi kuwa kiongozi wao mpya .

  Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi wa kundi la Kijihad la Islamic State (IS) na mtu ambaye alikuwa akisakwa sana duniani , alijiua kufuatia uvamizi wa Marekani uliotekelezwa na kikosi maalum cha wanajeshi kaskazini magharibi mwa Syria.

  Kiongozi huyo aliyejiita 'Kalifa Ibrahim' alikuwa amewekewa dola milioni 25 kwa mtu yeyote ambaye angefichua maficho yake na alikuwa akisakwa na Marekani na washirika wake tangu kuanzishwa kwa kundi la IS miaka mitano iliopita.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako