• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 4-Januari 10)

    (GMT+08:00) 2020-01-10 19:15:46

    Waziri Mkuu Tanzania,Kassim Majaliwa afuta mnada wa nafaka

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu zilizofanyika awali.

    Mnada huo ambao unahusisha mahindi tani 5,000 na ngano tani 460.12 unafanyika baada ya wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha, hivyo Serikali imeamua kuuza ili kufidia gharama zake. Nafaka hizo ziliingia nchini Machi 2017.

    Waziri Mkuu Majaliwa alisitisha mnada huo siku ya Alhamisi, Januari 9, 2020 wakati akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Bw. Ben Asubisye, ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.

    Waziri Mkuu ameagiza kutangazwa upya kwa mnada mwingine wa kuuza mahindi hayo sambamba na ngano na wahakikishe masuala yote kuhusu mnada huo yanakamilika ndani ya siku tatu kuanzia leo tarehe 09 Januari 2020.

    Kadhalika, Majaliwa ameutaka uongozi wa TRA uhakikishe mnada unaofuata unakuwa wa wazi, huru pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa wananchi wote kushiriki ili kuondoa malalamiko.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako