• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 4-Januari 10)

    (GMT+08:00) 2020-01-10 19:15:46

    Rais wa Marekani Donald Trump asema Iran yaacha kushambulia ngome za Marekani

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema Iran "inaonekana kurudi nyuma"baada ya kufyatua makombora dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.

    Bw.Trump, alisema kuwa hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo.

    Kambi za kijeshi za Irbil na Al Asad zilishambuliwa mapema Jumatano alfajiri. Iran ilisema ilichukua hatua hiyo kulipiza kisasi mauaji ya wiki iliyopita ya jenerali wake wa ngazi ya juu Qasem Soleimani.

    Ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ililenga msafara wake akiwa na maafisa wa wakuu wa kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran,mjini Baghdad katika hatua ambayo ilizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.

    Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa "kofi la usoni" kwa Marekani na kutoa wito kwa nchi hiyo kuondoka mashariki ya kati.

    Shambulio dhidi ya Soleimani pia liliwaua wanachama wa kundi la waasi wanaounga mkono Iran ambao pia wamesema watalipiza kisasi.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako