• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 4-Januari 10)

    (GMT+08:00) 2020-01-10 19:15:46

    Bei ya mafuta yapanda kutokana na shambulizi la Iran

    Gharama za mafuta ghafi katika soko la kimataifa zimepanda,mara tu baada ya kambi mbili za majeshi ya Marekani nchini Iraq kushambuliwa na makombora.

    Inaelezwa bei ya mafuta ghafla imepanda kwa asilimia 1.4 ,sasa ikiuzwa kwa dola za Marekani 69.21 kwa pipa moja.

    Wakati tukio linatokea,hali ya mzozo katika ukanda wa Mashariki ya Kati ,inaeleza gharama ya mafuta kwenye soko la dunia zilishuka kutokana na mzozo uliopo katika ukanda wa mashariki ya kati.

    Shambulio hilo lilikuwa ni kisasi baada ya kuuawa kwa kamanda wa juu wa jeshi la nchi hiyo Qaseem Soleimani,lililotokea baada ya shughuli za mazishi ya Soleimani,aliyeuawa na shambulio la Marekani siku ya ijumaa wiki iliyopita.

    Hali hii inaelezwa kuwa inaweza kuathiri usafirishaji wa mafuta kupitia lango la Hormuzlinalotenganisha Ghuba ya Uajemi na Oman.

    Takriban asilimia 20 ya mafuta duniani husafirishwa kupitia lango hilo linalounganisha eneo la ghuba na bahari ya Arabia.

    Mlango wa Hormuz ni muhimu kwa wasafirishaji wakubwa wa mafuta katika eneo la ghuba-Saudi Arabia,Iraq,Umoja wa Falme za Kiarabu na Kuwait,ambazo uchumi wao unajengwa kutokana na uzalishaji mafuta na gesi.

    Iran pia inategemea kwa kiasi kikubwa njia hiyo kwa ajili ya kusafirisha mafuta.

    Taifa la Qatar,ambalo ni mzalishaji mkubwa wa gesi duniani,husafirisha karibu gesi yake yote kupitia lango hilo.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako