• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 11-Januari 17)

  (GMT+08:00) 2020-01-17 18:57:01

  Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema wale waliohusika katika kuidungua ndege Ukraine ni lazima waadhibiwe

  Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema wale waliohusika katika kuidungua ndege ya abiria ya Ukraine ni lazima waadhibiwe.

  Katika hotuba iliyopeperushwa kwenye televisheni ya taifa rais huyo amesema wale waliofanya kosa hilo ni sharti wahukumiwe.

  Aidha amesema tukio hilo lililosababisha mauaji ya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo litafanyiwa uchunguzi wa kina ambapo ameitaka idara ya mahakama nchini humo kubuni jopo maalum lenye majaji wa ngazi ya juu na wataalam akidai kwamba ulimwengu utakuwa ukitazama.

  Msemaji wa idara ya mahakama ya Iran amesema tayari kuna watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako