• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 11-Januari 17)

  (GMT+08:00) 2020-01-17 18:57:01

  Baba adaiwa kumuua mtoto wake mwenye miaka miwili baada ya kujisaidia kitandani

  Juma Daniel wa miaka 30, amuua mtoto wake wa miaka miwili baada ya kujisaidia haja kubwa kitandani.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema, Daniel ambaye ametengana na mzazi mwenzake, alikuwa amelala na mtoto huyo.

  Baba huyo anasemekana alimchoma choma moto kwa kutumia kitu cha ncha kali usoni, makalio, na sehemu nyingine za mwili na kumsababishia majeraha makali.

  Mbali na baba huyo kumjeruhi vibaya mtoto huyo, bado haliendelea kumficha ndani na kuendelea kumtibu kwa miti shamba hadi afya ya mtoto ilipokuwa mbaya zaidi ndipo mtuhumiwa aliamua kutoroka.

  Baba wa mtoto kutoweka nyumbani, majirani walisikia sauti ya mtoto huyo akiomba msaada, ndipo walipoingia ndani ya nyumba na kugundua mtoto huyo amejeruhiwa vibaya na kuripoti tukio hilo uongozi wa kijiji.

  Mtoto huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali kwenye matibabu kutokana na majeraha makubwa ya kuchomwa moto.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako