• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 18-Januari 24)

    (GMT+08:00) 2020-01-24 18:57:19

    Uingereza yaahidi kukoma kutoa tahadhari ya usafiri Kenya.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amemhakikishia Rais Uhuru Kenyatta kwamba taifa hilo litaacha kutoa tahadhari za usafiri dhidi ya Kenya kwani hatua hiyo huathiri uchumi wa nchi.

    Walipokutana Jumanne katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyo katika barabara ya No.10 Downing jijini London, wawili hao walijadili madhara ya taarifa hizo ambazo mara nyingi hutolewa panapotokea shambulio la kigaidi nchini.

    Rais Kenyatta alimshukuru Waziri Mkuu Johnson kwa kutambua athari za taarifa hizo za kusafiri pamoja na hakikisho la Bw Johnson kwamba taarifa hizo hazitatolewa tena dhidi ya Kenya.

    Walikubaliana kwamba Kenya na Uingereza sharti zishirikiane zaidi katika vita dhidi ya ugaidi.

    Bw Johnson alisema anatambua kwamba Kenya imeathirika sana kutokana na ugaidi na hivyo kuna haja ya kushirikisha juhudi kuukabili uovu huo.

    Alisema kambi ya Uingereza ya mafunzo ya kijeshi iliyo Nanyuki itaendelea kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Kenya kama njia ya kuimarsiha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili.

    Kando na hayo, walijadili jinsi biashara itakavyokuwa baada ya Uingereza kujiondoa katika Muungano wa Ulaya.

    Rais alikuwa ameandamana na Mawaziri Ukur Yatani, Monica Juma na Adan Mohammed pamoja na Balozi wa Kenya nchini Uingereza Manoah Esipisu.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako