• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 18-Januari 24)

  (GMT+08:00) 2020-01-24 18:57:19

  Mwanamke tajiri zaidi Afrika afunguliwa mashtaka ya ulaghai….Angola

  Taifa la Angola limemfungulia mashtaka ya ulaghai, mwanamke tajiri zaidi barani Afrika Isabel Dos Santos. Hii ni baada ya kutuhumiwa kulipora taifa hilo.

  Mwanasheria mkuu Helder Pitta Groz alisema kwamba madai hayo yanahusiana na wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Sonangol. Isabel dos Santos anatuhumiwa kwa usimamizi na ufujaji wa fedha wakati alipokuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo ya Sonangol. Amefungliwa mashtaka ya usimamizi mbaya wa ofisi , kutumia ushawishi wake na kughushi stakhabadhi miongoni mwa uhalifu mwengine wa kiuchumi.

  Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la BBC, uchunguzi kuhusiana na usimamizi wake wa kipindi cha miezi 18 katika kampuni hiyo ya mafuta kuanzia mwezi Juni 2016 ulianzishwa baada ya mrithi wake Carlos Satumino kuelezea mamlaka kuhusu uhamishaji wa fedha usio wa kawaida .

  Stakhabadhi zilivuja wiki hii zikidai kwamba bi Dos Santos , mwana wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos , alijipatia mali ya thamni ya dola bilibo 2.1 kwa kulipora taifa lake. Amekana madai.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako