• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 18-Januari 24)

  (GMT+08:00) 2020-01-24 18:57:19

  Nkurunziza kupata donge nono atakapostaafu mwezi Mei..Burundi

  Bunge la Burundi limepitisha sheria inayotoa idhini kwa serikali ya nchi hiyo kumlipa Rais Pierre Nkurunziza Sh53 milioni (dola za Amerika 530,000) atakapoondoka afisini. Rais huyo ameahidi kutowania urais kwa mara nyingine katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Mei 2020.

  Mnamo Juni 7, 2018, Nkurunziza akiwa jijini Gitega alitia saini uidhinishaji wa Katiba Mpya iliyopitishwa kupitia kura ya maamuzi iliyofanyika Mei 17, 2018, na ambayo ingemruhusu kuwania urais mwaka huu 2020 na kuhudumu kwa kipindi cha miaka saba. Ila sasa, amebadilisha uamuzi huo.

  Kwa mujibu wa sheria hiyo, Nkurunziza pia atakuwa akipokea mshahara hadi afe, nyumba ya kifahari na manufaa yote ambayo Makamu wa Rais hupata.

  Wabunge pia walipendekeza kuwa Rais huyo apandishwe hadhi na aitwe Kiongozi Mkuu (Supreme leader) na Shujaa wa uzalendo (Champion of patriotism).

  Kama kiongozi mkuu Nkurunziza bado anatarajiwa kuwa na mamlaka, hasa katika chama tawala, ambacho kinapigiwa upatu kushinda katika uchaguzi ujao.

  Wananchi wametoa hisia mseto kuhusu hatua ya malipo ambayo Rais huyo atapokea baada ya kustaafu.

  Wengine walikosoa hatua hiyo ya bunge ikizingatiwa kuwa taifa hilo ni mojawapo ya mataifa maskini duniani.

  Lakini wengine walisema kuwa manufaa hayo yanafaa kama asante kwa Nkurunziza ambaye ametumikia taifa hilo katika cheo hicho cha juu.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako