• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 25-Januari 31)

  (GMT+08:00) 2020-01-31 20:40:52

  Kenya Airway yasitisha safari zake China

  Shirika la ndege la Kenya limetangaza kusitisha safari zake kwenda China kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.

  Virusi hivyo vimesababisha vifo 213 nchini China na maambukizi kwenye mataifa mengine 16.

  Visa sita vya maambukizi vimeripotiwa barani Afrika ingawa wagonjwa waliofanyiwa vipimo wamekutwa kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo.

  Jumanne wiki hii nchini Kenya, mwanafunzi aliwekwa karantini hospitalini katika mji mkuu Nairobi, baada ya mwanafunzi huyo kutokea katika mji wa Wuhan nchini China, eneo ambalo ndio chimbuko la mlipuko huo.

  Kenya Airways imesema kuwa bado iko kwenye mazungumzo na wizara ya afya na wizara ya mambo ya nje kuhusu muda ambao ndege hizo zitaanza safari ya China.

  Lakini safari za mji mkuu wa Thailand, Bangkok, zitakuwa zinaendelea.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako