• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (February 1-February 7)

    (GMT+08:00) 2020-02-07 20:11:32
    Rais Mstaafu wa Kenya,Daniel Moi aaga dunia

    Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi alifariki dunia akiwa na miaka 95.

    Rais mstaafu alifariki katika Hospitali ya Nairobi mapema asubuhi ya tarehe Februari 4 akiwa na familia yake.

    Kwa zaidi ya robo karne Daniel arap Moi alitawala siasa za Kenya. Yeye alikuwa mwanasiasa aliyetaka kupendwa zaidi na wananchi kuliko alivyokuwa mtangulizi wake, rais wa kwanza wa jamuhuri ya Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

    Moi alizaliwa Septemba 2, mwaka 1924, katika jamii ya wakulima katika kaunti ya Baringo, katikati magharibi mwa Kenya.

    Jina lake la kwanza lilikuwa Toroiticha arap (mwana wa) Moi lakini baadaye akabatizwa katika Ukristo na kupewa jina la Daniel. Alipewa jina hilo la Wamishenari Wakristo akiwa mwanafunzi.

    Moi alikuwa mmoja wa mwanasiasa wachache mashuhuri waliofanikiwa, ambaye hakutoka katika mojawapo ya makabila mawili makubwa nchini Kenya – Wajaluo na Wakikuyu. Alitoka jamii ndogo ya Tugen, mojawapo wa makundi yanayounganisha kabila kubwa la Wakalenjin.

    Alianza kufanya kazi kama mwalimu mwaka wa 1945 katika shule ya African Government School na mwaka mmoja baadaye akiwa na umri wa miaka 22 akateuliwa kuwa mwalimu mkuu,na mwaka 1978 akawa Rais baada ya aliyekuwa Rais Jomo Kenyatta kufariki.

    Moi aliliongoza taifa la Kenya kama Rais kutoka 1978 hadi 2002.


    1  2  3  4  5  6  7  8  9  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako